Jiko Letu

Kuhusu Jiko Letu

Jiko Letu ni mkusanyiko wa mapishi ya nyumbani ya Tanzania na Afrika Mashariki, yaliyoandikwa kwa Kiswahili rahisi, hatua kwa hatua.

Picha na mapishi ni yetu au ya wapishi waliotupa ruhusa, na majina yao yanaonyeshwa kwenye kila pishi. Ukiona kazi yako hapa bila ruhusa yako, tuandikie tutaiondoa mara moja.

Una pishi lako ungependa tuliweke? Tutumie kwa barua pepe hapa chini.

Wasiliana nasi

Sera ya Faragha (Privacy Policy)

Imesasishwa: 26 Nov 2026

Taarifa tunazokusanya: hatukuombi jina, namba ya simu, barua pepe wala akaunti. Ukiwasha arifa, tunahifadhi token ya arifa (namba maalum inayotolewa na Google Firebase) pamoja na aina za arifa ulizochagua. Hivyo ndivyo tunavyoweza kukutumia arifa.

Vipendwa na alama za viungo huhifadhiwa kwenye simu yako tu. Hatuzipokei.

Tunavyotumia taarifa: kukutumia arifa ulizochagua tu. Hatuuzi wala kushiriki taarifa hizi na mtu mwingine.

Huduma za watu wengine: tunatumia Google Firebase Cloud Messaging kutuma arifa. Google huchakata token kwa mujibu wa sera yao ya faragha (policies.google.com/privacy).

Kufuta taarifa: ukizima arifa kwenye mipangilio ya simu au ukiondoa app, token yako huacha kufanya kazi na tunaifuta kwenye mfumo wetu. Unaweza pia kutuandikia tuifute.

Watoto: huduma hii haijalenga watoto walio chini ya miaka 13.